NEWS

Former Tanzanian President, Honorable Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, visits BintiAfrica Company Limited To observe Where his shirts are being Tailored

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania.

Akizungumza na Michuzi TV, Dkt. Kiwete amesema kuwa Binti Afrika imemshonea nguo muda mrefu kwa ubunifu wa hali juu, amepongeza kwa kuwa nguo hizo za aina ya Batiki zina viwango vya ubora zinazoweza kuuzika kokote duniani.


Dkt. Kikwete amepongeza Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Johari Sadiq licha ya mchango kutoka kwa Mama yake mzazi, kwa kujituma na ubunifu huo ambapo unaweza kutengeza mazingira yoyote kujipatia kipato. “Watu wakumbuke Wabunifu wapo hapa nchini, wasifikirie vitu vya nje peke yake hapa ndani (Tanzania) wanaweza kupata vitu vyenye ubora wa hali ya juu”,amesema Dkt. Kikwete.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji Nguo, Johari Sadiq amesema wamepata heshima kubwa kupata ugeni wa Dkt. Kikwete katika Kiwanda hiko amesema hatua hiyo imetokana na ubora na ubunifu walionao hivyo imepelekea kuwa mteja wao muda mrefu. 


“Dkt. Kikwete amekuwa mteja wetu toka alipokuwa Rais wa nchi hii, tumeanza kuvalisha nguo zetu toka mwaka 2013, alinikuta kwenye Maonyesho nikiwa na bidhaa zangu akazipenda ubora wake, akajaribu kwa kuagiza Shati mbili”, amesema Johari


Johari amesema kuwa amekuwa akijifunza muda mrefu kwa watu wengine ambapo wamefanya kazi hiyo ya ubunifu kwa muda mrefu.Ametoa wito kwa Wabunifu kutofautisha ubunifu wa majukwaani na uzalishaji nguo kuweka msingi wa uzalishaji wakuvaa nguo za kila siku, ametoa wito kwa Wabunifu kujikita zaidi kwenye uzalishaji zaidi wa nguo. Amesema miaka mitano anataka kuwa na ‘Brand’ ambayo itatambulika zaidi nchini kwa kuvalisha viongozi na watu wakawaida. 

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya  kutembelea Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia nguo zinazo tengenezwa na  Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania. kulia ni MKurungezi wa kiwanda hicho, Johari Amour Sadiq.

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mashine mbalimbali  katika Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.

Mafundi wa  Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa wakiendelea na kazi.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa kiwanda  cha nguo cha Binti Africa leo jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *