NEWS

Tanzanian Designer dressing up Presidents

Johari Sadiq ni mmoja kati ya vijana wa Kitanzania wanaojishughulisha na ubunifu wa mavazi ambapo pia anamiliki kiwanda chake cha Nguo cha Binti Africa.

Mbunifu huyo ambaye amekuwa akiwavisha watu maarufu nchini akiwemo Rais mstaafu Jakaya Kikwete na Rais John Magufuli anasema haikuwa safari fupi hadi kufikia hatua hiyo kwani alipitia changamoto nyingi.

“Nilijikita kwenye ushonaji kupitia mama yangu, niliona kama ni fursa ambapo wakati huo nilikuwa nimeajiriwa mwaka 2011 ambapo nikasema niache kuajiriwa na kujikita huku na nilianza na mtaji wa Shilingi Elfu Arobaini,”amesema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *